Saturday, January 8, 2011

We say boldly to Kikwete, NO, but NO THANK YOU!

Bunge ni mhimili wa dola unaofanya kazi kwa niaba ya wananchi. Hoja binafsi ya katiba mpya imewasilishwa bungeni, na huko ndiko kutaundwa baraza la kutunga katiba, na watakaofanya hivyo ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wawakilishi wao bila kuingiliwa na Serikali. 
Na ni huko pia ambapo makundi mbalimbali ya jamii yatashirikishwa katika mchakato wa kuandikwa katiba mpya na USHIRIKI huo hautakuwa kwa hisani ya RAIS Kikwete kupitia wateule wake.
Tunampongeza kwa KUKUBALI KATIBA MPYA.
Lakini si kazi yako Mhe. Rais na wala si kazi ya Serikali yako, ni kazi ya Bunge, ni kazi ya Wananchi wa Jamhuri ya Tanzania.
Si sahihi kwa  kuunda kwako tume, na pia si njia sahihi ya kupata katiba mpya tunayoitaka. 
Huku ni kuteka nyara hoja ya watu, hii si kazi yako, hatujakutuma!

A DECENT CALL

Your Excellency Mr. President, to your endorsement for New Constitution, WE SUPPORT YOU!

Your involvement with the so called "Constitutional Review Commission"

WE BOLDLY SAY, NO, BUT NO THANK YOU